Home Jamii RAIS MWINYI AHIMIZA AMANI NA USHIRIKIANO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU.

RAIS MWINYI AHIMIZA AMANI NA USHIRIKIANO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU.

27
2

Na Siti Ali, Kizimbani Dole,25 Oktoba 2025.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewahakikishia wananchi kuwa serikali imejipanga kuhakikisha ulinzi wa kutosha katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu,

Akizungumza katika dua ya kuliombea Amani taifa yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Makanisa Zanzibar, yaliyofanyika Uwanja wa Michezo wa Kizimbani Dole, Mkoa wa Mjini Magharibi, Dkt. Mwinyi amesema serikali zote mbili zimejiandaa kuhakikisha kila Mtanzania mwenye sifa ya kupiga kura anapata fursa ya kutekeleza haki yake ya msingi ya kikatiba.

“Amani, Muungano na Mshikamano ni tunu za Taifa ambazo CCM itaendelea kuzilinda kwa maslahi ya wananchi wote bila ubaguzi wa asili wala dini,” amesema Rais Mwinyi.

Aidha, amesisitiza kuwa serikali itaendelea kudumisha uhuru wa kuabudu kwa waumini wa dini zote, sambamba na kuimarisha ushirikiano na taasisi za kidini katika sekta za elimu, afya na maji.

Rais Mwinyi almeishukuru Jumuiya ya Makanisa Zanzibar kwa kuandaa maombi hayo ya amani, na kusema hatua hiyo inaonesha uzalendo na upendo kwa nchi. “Taasisi za kidini zina jukumu kubwa la kuwaandaa waumini kuwa raia wema na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa,” ameongeza.

Maombi hayo ya amani yalikutanisha viongozi wa dini, watumishi wa serikali na wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Unguja, kaw lengo la kupata amani ya kudumu kuelekea uchaguzi mkuu oktoba 29 2025.

2 COMMENTS

Leave a Reply to amai ni msingi wa maendeleo Cancel reply

Please enter your comment!
Please enter your name here