Na Said Khamis, Wilaya ya Kati.18/11/2025.
Licha ya kuwepo kwa viashiria vya alama za barabarani katika maeneo mbalimbali ya barabara za mjini na vijijini bado baadhi ya madereva wanaoendesha vyombo vya moto hushindwa kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani.
Wakizungumzana na TOZ wananchi wa shehia ya Jendelee njia ya Cheju, wamesema baadhi ya madereva huendesha vyombo kwa mwendo kasi bila ya kuzingatia alama za barabarani hali inayohatarisha usalama wa maisha yao.
Walisema katika njia hiyo ya cheju pana skuli ya jendele ambayo kuna muda wamapumziko na muda wakutoka skuli huvuka njia hiyo lakini badhi ya madereva hushindwa kuzingatia alama zilizoekwa.

‘’Barabara yetu ni kubwa zinapita gari aina mbalimbali lakini magari makubwa yanapofika eneo la skuli kuna zebra lakini bado wanaendesha mwendo wa kasi na ukizingatia kuna watoto wadogo waskuli ambao bado uwelewa wao mdogo kufahamu kutembea njiani kwa tahadhari’’ walisema wananchi
Nae sheha wa shehia ya jendele Zidi Suleiman Abjeidi ameeleza kuwa changamoto hiyo tayari ameshaifikisha sehemu husika kwa lengo la kupatiwa ufumbuzi.
Sambamba na hayo amewaomba madereva hao kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani ili kuweza kuepukana na ajali zinazoweza kuepukika.

‘’Tayari tumeshaiyandikia barua mamlaka zinazohusika ili kutufanyia utaratibu wakutuekea matuta, maana kumewekwa zebra lakini baadhi ya madereva wanashindwa kuziheshimu alama hizo’’ alisema Sheha
Akitolea ufafanuzi kuhusiana na kadhia hiyo inayojitokeza katika barabara nyingi si ya Cheju tu pekee Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano kutoka Mamlaka ya Usafiri na Usalama Barabarani Zanzibar Hakimu Daudi Mwita alisema wanapogundua baadhi ya madereva wanakiuka sheria za usalama barabarani hushirikiana na jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani ili kuwatia hatiani wale wote wanaokiuka sheria hizo.

‘’Malalamiko hayo tunayapata sehemu nyingi kwamba baadhi ya madereva hawafuati alama za barabari hilo nijukumu letu kuhakikisha tunawachukulia hatua wale wasiofuata sheria za barabarani’’ alisema Hakim
Aidha Hakimu amewataka madereva wote kufuata sheria na kanuni zilizoekwa na mamlaka ya usafiri na usalama barabarani ili kuepukana na ajali za mara kwa mara.






















Submit thetimesofzanzibar.com for GoogleSearchIndex to have it displayed in web search results.
Add thetimesofzanzibar.com now at https://searchregister.org
Hello,
Add thetimesofzanzibar.com to SEODIRECTORY fort a better ranking in Web Search results order.
https://seodir.pro
More and more people skip Google Search and ask ChatGPT to search for everything.
Add thetimesofzanzibar.com to our AI-optimized directory now to increase your chances of being recommended.
Join now: https://AIREG.pro/
Hi https://thetimesofzanzibar.com/how-to-travel-fashionably-on-a-long-flight/,
I hope you’re doing well.
I came across your business online and thought you might be interested in improving your visibility and traffic on search engines.We specialize in helping businesses strengthen their online presence through effective SEO strategies.
Once you share your target keywords and target market, I’ll send a full proposal.
Warm regards,
Sonam