Home Jamii WADAU WA UCHUMI BULUU WAOMBA TOZO RAFIKI KWA WAGENI WANAOTEMBELEA MAENEO YA...

WADAU WA UCHUMI BULUU WAOMBA TOZO RAFIKI KWA WAGENI WANAOTEMBELEA MAENEO YA BAHARI

29
0

Wadau wa sekta ya Uchumi nchini wameiomba Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi kuweka tozo rafiki kwa wageni wanaotembelea maeneo ya bahari, ili kuendana na kasi ya ukuaji wa sekta hiyo nchini.

Wakizungumza katika mkutano wa wadau kuhusu tozo mpya kwa wageni wanaotembelea eneo la hifadhi ya Bahari ya PECCA, uliofanyika katika ukumbi wa Kilimo Wete, Kaskazini Pemba, wadau hao wamesema ni muhimu kuendelea kutoa elimu kwao juu ya tozo hizo mpya ili waweze kuelewa kwa undani lengo na manufaa yake.

Mmoja wa wadau, Khamis Said Makame, amesema kuwa tozo hizo zinapaswa kuzingatia mazingira halisi ya uwekezaji na utalii wa baharini, ili zisiwe mzigo kwa wawekezaji na watalii wanaotembelea maeneo hayo. Nae Said Mbarouk Hassan, Meneja wa Moon Light, amesema kuwa elimu ya kutosha kwa wadau ni muhimu ili kuwe na uelewa wa pamoja kuhusu utekelezaji wa tozo hizo.

Kwa upande wake, Meneja wa PECCA, Shafii Khamis Soud, amesema kuwa lengo la tozo hizo ni kuboresha huduma katika maeneo ya ukanda wa PECCA na ya baharini yanatunzwa ipasavyo,” amesema Shafii.

Akifungua mkutano huo, Afisa Mdhamini wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Dk. Salim Mohammed Hamza, amesema jukumu la wizara ni kusimamia utekelezaji wa sheria mpya ya tozo hizo, ambapo kutakuwa na vituo maalum vitakavyohusika kukusanya mapato hayo.

“Serikali imeweka utaratibu maalum wa ukusanyaji wa tozo hizi kwa uwazi, ili fedha zitakazopatikana ziweze kutumika kuboresha zaidi sekta ya uchumi buluu,” amesema Dk. Salim.

Naye Mayasa Abdalla, Afisa Mkuu wa Idara ya Uvuvi Pemba, amesema mkutano huo umelenga kujenga uelewa wa pamoja kati ya serikali na wadau ili kuhakikisha utekelezaji wa tozo hizo unakwenda sambamba na malengo ya kukuza uchumi wa buluu Zanzibarkuongeza thamani ya hifadhi hizo za baharini.

“Tozo hizi si kwa ajili ya kikwazo, bali ni njia ya kuhakikisha huduma zinaboreshwa na mazingira

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here