Home Lifestyle Afya WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUTUMIA FURSA ZA MAENDELEO KUTETEA HAKI ZA WATU...

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUTUMIA FURSA ZA MAENDELEO KUTETEA HAKI ZA WATU WENYE ULEMAVU

30
0

Na Mwandishi wetu Mkoa wa Kusini Unguja, Novemba 11,2025.

Waandishi wa habari wameshauriwa kuzitumia fursa wanazozipata juu ya utekelezaji wa maendeleo kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Ushauri huo umetolewa na Mkufunzi Haji Nassor wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA Zanzibar huko Tunguu.

Amesema ni vyema waandishi wa habari kutumia mbinu mbali mbali za kupata taarifa sahihi ambazo zitaleta faida na maendeleo ikiwemo kutumia vyanzo sahihi vya kupata taarifa ikiwemo katiba ya Zanzibar, pamoja na sheria za watu wenye ulemavu .

Aidha amewaomba waandishi wa habari na jamii kwa ujumla kuacha kuwatolea mfano wa majina mabaya watu wenye ulemavu kwani hupelekea athari kubwa kwa watoto na familia.

Nae Afisa program mwandamizi wa Baraza la habari Tanzania (MCT) Shifaa Said Hassan amewasihi waandishi wa habari kuendelea kujifunza mambo yatakayowasaidia katika uchambuzi wa habari na kufanya utafiti wa kina juu ya habari zao ili kuibua changamoto za watu wenye ulemvu kwa usahihi.  

Akifungua mafunzo hayo Meneja mahusiano wa Chama cha wandishi wa habari wanawake TAMWA Zanzibar Sofia Ngalapi amesema waandishi wa habari wamefanya kazi kubwa ya kuibua changamoto za watu wenye ulemavu na kuendelea kutumia sera, mikataba na sharia ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Kwa upande wake afisa program wa TAMWA Khairat Ali amesema kuelekea siku ya watu wenye ulemavu duniani ni vyema waandishi kuangalia watu wenye ulemavu wanakabiliwa na changamoto na kuzipatia ufumbuzi sambamba na kuitumia vyema mtandao ya kijamii.

Nao waandishi wa habari wameiomba jamii na viongozi wa taasisi kutoa ushirikiano ili kufanya kazi kwa urahisi pamoja na kuwaunga mkono watu wenye ulemavu juu ya harakati zao za kila siku.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here