Home Uchumi Fedha VIJANA WATAKIWA KUTUMIA MAJUKWAA YA KIMTANDAO KUPATA FURSA ZA MASOKO.

VIJANA WATAKIWA KUTUMIA MAJUKWAA YA KIMTANDAO KUPATA FURSA ZA MASOKO.

18
0

Na Siti Ali.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Vijana Zanzibar Ali Haji Hassan ametoa wito kwa Wahitimu wa Mafunzo ya Vijana Viongozi kuyatumia mafunzo na Majukwaa ya Kimtandao katika kukuza na kupata fursa za masoko ya Biashara.

Akizungumza katika mahafali hayo ya Vijana Viongozi katika Ukumbi wa Zanzibar Youth Initiative uliopo Mpendae Zanzibar amesema wakati umefika wa Vijana kutumia Mitandao kuwa ni fursa ya Kutangaza biashara wanazozifanya jambo litakalowasaidia kuongeza wateja na kujiongezea kipato.

Aidha amesema amefurahishwa na utendaji kazi wa Vijana hao licha ya uchache wao ila wameweza kuwafikia Vijana 968 kwa Unguja na Pemba jambo ambalo limeenda kubadilisha mitizamo ya Vijana kuhusu biashara ya Mtandao hali itakayosaidia kukuza Uongozi Jumuishi na Uwezeshaji wa Kiuchumi kwa Vijana.

Amewasisitiza wahitimu kuyatumia mafunzo hayo na kuwa mfano wa kuigwa na Vijana wengine pamoja na kuzitumia vyema fursa walizozipata kupitia mafunzo hayo.

Akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa Pamoja Youth Initiative Rashid Mwinyi amewataka Vijana kufahamu kuwa safari ya mafanikio ina kuja kwa jitihada na kuzikabibili changamoto mbalimbali watakazokumbana nazo

Aidha kuzitumia fursa walioipata ya kupata mafunzo hayo kwa kuyatumia katika kukuza mitaji na biashara zao sambamba na kuwasaidia Vijana watakaohitaji Ujuzi huo na kufanya kazi kwa mashirikiano

Pia amefahamisha kuwa kupitia program hiyo iliwaunganisha Vijana hao na Wadau na taasisi muhimu za kifedha na kibiashara ikiwa ni pamoja na ZEEA, CRDB Bank, TCB Bank, NMB Bank, TCB Bank na Mix by Yas.

Amesema kupitia ushirikiano huo Vijana hao walipata fursa ya kujifunza masuala ya Fedha, usimamazi wa biashara, matumizi ya mifumo ya Kidijitali katika kutunza kumbukumbu, kutunza biashara mtandaoni, kuandaa mipanga ya biashara na kuimarisha mifumo ya usimamizi wa fedha.

Pia amefahamisha kuwa Taasisi hiyo ipo tayari kushirikiana wadau mbalimbali katika kuhakikisha Vijana wanatumia Majukwaa ya Kimtandao Vizuri na sio kutumia majukwaa hayo kuwa chanzo cha kuharibu jamii hasa Vijana.

Akisoma Risala kwa niaba ya Wahitimu hao Salmin Amour Mohammed amesema Mradi huo umewasaidia Kuwajenga kuwa Wajasiri, kujiamini, kuongoza Vijana katika kutatua changamoto zao kibiashara na stadi za maisha kwa ujumla.

Aidha wameahidi kuyatumia mafunzo hayo walioyopata kuhakikisha wanafikia matarajio yao yataenda kuwa faraja kwao na kutimiza ndoto zao pamoja na Vijana wengine.

Mradi huo wa Going Beyond ambao upo chini ya Digital Opportunity Trust kwa mashirikiano na Mastercard Foundation ambao unatekelezwa na Taasisi ya Pamoja Youth Initiative ambapo jumla ya Vijana 12 kutoka Unguja na Pemba wamepatiwa mafunzo hayo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here