Home Jamii UWEKAJI JIWE LA MSINGI NYUMBA ZA BEI NAFUU CHUMBUNI

UWEKAJI JIWE LA MSINGI NYUMBA ZA BEI NAFUU CHUMBUNI

18
0


Na Siti Ali
Waziri wa nchi afisi ya raisi tawala za mikoa na idara maalumu za smz Mh Idrisa kitwana Mustafa amesema kuwa serikali ya zanzibar inaendelea kuchukuwa jitihada za mbali mbali kujenga nyumba za maendeleo za bei nafuu ili kuleta mabadiliko katika nchi na taifa kwa ujumla.

Ameyasema hayo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi wa nyumba za maendeleo huko chumbuni amesema kuwa mradi huo utakapomalizika utaleta mabadiliko makubwa kwa wananchi pamoja na kuuweka mji kuwa na taswira nzuri na yenye kuvutia.
Aidha amefafanuwa kuwa lengo la mradi huo ni kuondowa changamoto za makazi kwa wananchi kwani serikali itahkikisha inawapatia nyumba bora za makazi kwa maeneo ya unguja na pemba kwa jitihada za wizara husika sambamba na kusema kuwa
shirika la nyumba zanzibar limekuwa likitafuta mbinu mbali mbali ili wananchi kunufaika na nyumba hizo kwa utaratibu maalumu wa kulipa kwa awamu hadi apokamilisha malipo yake .

Mkurugenzi mkuu shirika la nyumba zanzibar sultan saidi suleiman amesema kuwa mradhi huu unahusisha nyumba 3000katika awamu ya kwanza nyumba 1,095 zinajengwa kupitia majengo 22ya horifa nne kwa gharama ya shilingi za kitanzania bilioni145.6sawa na dola za marekani milioni55.9ambapo mshaurj elekezi ni wakala wa majengo zanzibar ZBA.

Naibu waziri wa ardhi na maendeleo ya makazi salha mwinjuma ameeleza kuwa hii ni moja ya mikakati ya kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi ya kuanzisha miji ya kisasa yenye mahitaji yote muhimu ya kijamii sambamba
na kuwataka wakandarasi wanajenga kwa viwango na inamalizika kwa wakati uliopangwa
Asilimia aruubaini watakaokodishwa ni wanyonge waliokuwa na kipato cha chini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here