Home Siasa RAIS MWINYI AWATEUA WAJUMBE WAPYA WA BARAZA LA WAWAKILISHI

RAIS MWINYI AWATEUA WAJUMBE WAPYA WA BARAZA LA WAWAKILISHI

22
0

Na Mwandishi wetu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameteua majina mapya ya viongozi wa Baraza la Wawakilishi. Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 06 Novemba 2025 na Ofisi ya Baraza la Mapinduzi kupitia taarifa rasmi kwa vyombo vya habari.

Katika uteuzi huo, jumla ya viongozi nane wameteuliwa kuungana na Baraza la Wawakilishi, hatua inayolenga kuimarisha uwakilishi, uwajibikaji na ufanisi katika kuisimamia serikali pamoja na masuala ya maendeleo ya wananchi. Miongoni mwa walioteuliwa ni Shariff Ali Shariff, Masoud Ali Mohammed, Dkt. Saada Mkuya Salum, Nadir Abdullatif Alwardy, Idrisa Kitwana Mustafa, Tawfik Salim Turky, Said Ali Juma pamoja na Dkt. Juma Malik Akil.

Uteuzi huo uneanza rasmi tarehe 06 Novemba 2025, na viongozi wote walioteuliwa wametakiwa kuripoti Barazani siku ya tarehe 07 Novemba 2025.

ikumbukwe kuwa uteuzi huu ni wa kikatiba unaompa mamlaka Rais wa Zanzibar kuteuwa wajumbe 10 wa Baraza la Wawakilishi, hatua inayolenga kuongeza ufanisi na kuhakikisha masuala ya wananchi yanapata sauti pana zaidi kupitia viongozi walioidhinishwa kisheria.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here