Home Siasa RAIS MWINYI AMUAPISHA MWANASHERIA MKUU WA ZANZIBAR.

RAIS MWINYI AMUAPISHA MWANASHERIA MKUU WA ZANZIBAR.

19
0

Na Siti Ali

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo tarehe 6 Novemba 2025, amemuapisha rasmi Dkt. Mwinyi Talib Haji kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar .

Uapisho huo umefanyika Ikulu Zanzibar. baada, Dkt. Mwinyi Talib Haji kuteuliwa tena kushika wadhifa huo ambao ameutumikia katika kipindi cha miaka mitano kilichopita.

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa ngazi za juu, akiwemo Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla, Mhandisi Zena Ahmed Said ambaye ni Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, pamoja na viongozi wa Serikali, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na viongozi wa dini.


.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here