Mgombea wa nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia ACT-Wazalendo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, amekutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya mawakala wa chama chake kwa upande wa Pemba.
Kikao hicho, ambacho ni awamu ya pili baada ya kile kilichofanyika hivi karibuni mjini Unguja, ambacho ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika katikati ya wiki ijayo. Kikao Kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi za chama hicho, mkoa wa kichama wa Chake Chake, Kusini Pemba.

Mawakala hao wamemuhakikishia mgombea wao utayari walionao, wakionesha mshikamano na uaminifu kwa chama chao kwa kufanya matembezi maalum ya kumuunga mkono na kusimamia haki zake hadi atakaposhinda nafasi hiyo muhimu kwa maslahi ya Wazanzibari wote.

Aidha, jioni ya leo, Mheshimiwa Othman anatarajiwa kuwahutubia wananchi, wanachama, wapenzi na wafuasi wa ACT-Wazalendo kupitia mkutano mkubwa wa hadhara wa kampeni utakaofanyika huko Wambaa, Jimbo la Chambani





















