Zanzibar, 18 Novemba 2025 .
Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar imetoa wito kwa Waislamu na wananchi kwa ujumla kuendelea kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema nyingi alizolijalia taifa, hususan neema ya amani na utulivu ambayo imeendelea kuliletea ustawi Zanzibar.
Katika taarifa kwa umma iliyotolewa na Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kaabi ameeleza kwamba siku za Jumatatu na Alhamis ni sunna kufunga. Hivyo amewataka Waislamu kushiriki ibada ya kufunga siku ya Jumatatu, tarehe 24 Novemba 2025, ambayo ni sawa na mwezi 3 Mfunguo Tisa mwaka 1447 Hijria. Ibada hiyo inalenga kumuomba Mwenyezi Mungu aliepushie taifa shari na kulipa neema ya kuendelea kuishi kwa utulivu.
Akinukuu hadithi ya Mtume Muhammad (S.A.W), Mufti amesema kuwa: “Watu wa aina tatu dua zao hazirejeshwi: Mfungaji mpaka atakapofungua…”, akiwasisitiza Waislamu kutumia siku hiyo kumuomba Allah alizidishe baraka na kuimarisha usalama wa nchi.
Aidha, Mufti ametoa mwito kwa Waislamu wote kushiriki katika dua maalumu ya kuliombea taifa amani na utulivu, itakayofanyika siku hiyo hiyo ya Jumatatu katika Msikiti wa Mwembe Shauri, mara tu baada ya Swala ya Adhuhuri.
Katika hatua nyingine, Mufti Mkuu amewakumbuka wanafunzi wote wanaoendelea na mitihani ya kidato cha nne, akimuomba Mwenyezi Mungu awape wepesi wa ufahamu, utulivu wa fikra, na mafanikio katika mitihani yao.
Taarifa hiyo imetolewa rasmi na Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanziba





















