Home Lifestyle Afya HUDUMA ZA AKINA MAMA NA WATOTO KUIMARIKA ZANZIBAR.

HUDUMA ZA AKINA MAMA NA WATOTO KUIMARIKA ZANZIBAR.

37
2

Na Siti Ali, 27 Oktoba 2025.

Serikali ithakikisha kila mwananchi anapata huduma bora za afya katika kila ngazi, hatua ambayo imeendelea kudhihirika kupitia miradi mikubwa ya ujenzi wa hospitali za Wilaya, Mikoa, Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja pamoja na Hospitali ya Saratani Binguni.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameyasema hayo katika hafla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo jipya la huduma za akina mama na watoto katika Hospitali ya Makunduchi, Mkoa wa Kusini Unguja .

Rais Dkt Mwinyi amesema Serikali itahakikisha inafanya kila jambo ili kunusuru maisha ya mama na mtoto, akisisitiza kuwa mafanikio ya sekta ya afya Zanzibar yanategemea nguvu ya pamoja kati ya Serikali, sekta binafsi na jamii. Hivyo ujenzi huo unatarajiwa kupunguza changamoto za uzazi na kuboresha huduma kwa wajawazito na watoto.

‘’Mradi huu mkubwa unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na wadau wa maendeleo, ukiungwa mkono na Fumba Port, Lady Fatuma Foundation na Jaffer Foundation, ambao wamejitokeza kusaidia kuinua huduma za afya kwa mama na mtoto’’

Aidhai Dkt. Mwinyi amewataka wananchi wa Makunduchi kuutunza mradi huo mara utakapokamilika, akibainisha kuwa Serikali itaendelea kusimamia ubora wa huduma za afya katika ngazi zote ili kila Mzanzibari apate tiba salama, bora na yenye viwango vya kimataifa.

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, wawakilishi wa taasisi za afya, wadau wa maendeleo pamoja na wananchi wa Makunduchi.

2 COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here