Home Uchumi Biashara DKT. MWINYI ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA BIASHARA, ATOA AHADI KUBWA KWA WAFANYABIASHARA

DKT. MWINYI ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA BIASHARA, ATOA AHADI KUBWA KWA WAFANYABIASHARA

61
0

Na Siti Ali.

Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameonesha kuridhishwa na hali ya biashara katika eneo la Darajani na kuahidi kuendelea kuboresha mazingira ya wafanyabiashara ili kukuza uchumi wa wananchi.

Dkt. Mwinyi amesema serikali imelenga kuliboresha zaidi eneo la Darajani kwa kujenga miundombinu ya kisasa kupitia mradi wa BIG Z, ambao utajumuisha ujenzi wa maduka pembezoni mwa barabara na kuongeza haiba ya mji wa Zanzibar. Aidha, amesema serikali itajenga maegesho ya kisasa katika eneo la Malindi na kupanua barabara ya Malindi–Mnazi Mmoja kuwa ya njia nne ili kurahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa.

Ameongeza kuwa serikali itaongeza fungu la fedha kwa ajili ya mikopo kwa wafanyabiashara na wajasiriamali, hasa wale waliokopa na kurejesha kwa wakati. Pia ameagiza ZECO kuweka transfoma mpya Darajani ili kumaliza changamoto ya umeme inayowakabili wafanyabiashara. Dkt. Mwinyi alisema serikali kwa kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi itatafuta njia za kupunguza kodi kwa wafanyabiashara ili kuwawezesha kuendesha biashara zao kwa ufanisi zaidi.

Rais Dkt. Mwinyi amewataka wananchi na wafanyabiashara kumpa kura nyingi ili aweze kuendeleza juhudi za maendeleo, amani na ustawi wa Zanzibar. Wafanyabiashara wa Darajani Souk nao wameeleza kunufaika na maboresho makubwa yaliyofanyika katika eneo hilo, ikiwemo mazingira bora ya biashara, kurejeshwa kwa kituo cha daladala, na uboreshaji wa bustani.

Kauli hiyo aliitoa alipokutana na wafanyabiashara na wajasiriamali wa soko la Darajani, akiwa katika mfululizo wa kampeni zake za kuomba kura na kuzungumza na makundi mbalimbali ya wananchi wa Zanzibar

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here