Home Siasa DKT. MWINYI AMUAPISHA HEMED SULEIMAN ABDULLA KUWA MAKAMU WA PILI WA RAIS...

DKT. MWINYI AMUAPISHA HEMED SULEIMAN ABDULLA KUWA MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR.

29
0

Na Siti Ali.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amemuapisha Mhe. Hemed Suleiman Abdulla kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameteuliwa kushika wadhifa huo kwa mara ya pili katika Awamu ya Nane ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Akizungumza baada ya kuapishwa, Makamu wa Pili wa Rais, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, ameahidi kuendeleza usimamizi wa utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na miradi yote ya maendeleo inayoendelea nchini kwa maslahi ya wananchi wa Zanzibar.

Aidha amesema kuwa Ilani ya 2020–2025 imetekelezwa kwa kiwango kikubwa, na kwamba Ilani mpya ya CCM ya 2025–2030 imekuja na mipango mikubwa zaidi ya kuipeleka Zanzibar hatua nyingine kimaendeleo.

sambamba na hilo amebainisha kuwa mipango hiyo inajumuisha miradi ya miundombinu, maboresho ya huduma za kijamii na maeneo mengine muhimu, na kusisitiza kuwa chini ya uongozi wa Rais Dkt. Mwinyi, atahakikisha mambo yote yaliyopangwa yanatekelezwa ipasavyo, na pale inapowezekana, kufanyika kwa kiwango cha juu zaidi kama ilivyokuwa katika kipindi cha kwanza.

Aidha, Mhe. Hemed aliwahimiza wananchi wa Zanzibar kuendeleza misingi ya amani, umoja na mshikamano, akivitaja kuwa nguzo kuu za mafanikio na ustawi wa taifa

Hafla ya uapisho umefanyika leo Ikulu Zanzibar, na imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, viongozi wa dini, Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na wanafamilia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here