Home Uchumi Biashara MAABARA YA UTAFITI WA AFYA YA WANYAMA ZANZIBAR, KUTOA HUDUMA ZA ...

MAABARA YA UTAFITI WA AFYA YA WANYAMA ZANZIBAR, KUTOA HUDUMA ZA VIWANGO VYA KIMATAIFA.

24
0

Na Saaid Khamis.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Mhe. Dkt. Haroun Ali Suleiman amesema Serikali kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti ya Friedrich Loeffler Institut (FLI) ya Ujerumani imeweza kufanikisha ujenzi wa Maabara ya Utafiti wa Afya ya Wanyama kwa lengo la kukuza Uchumu wa Nchi.

‎Ameyasema hayo katika Ufunguzi wa Maabara ya Utafiti wa Afya ya Wanyama la kisasa liliopo ZALIRI Dole-Kizimbani Mkoa wa Mjini Magharibi ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za kuadhimisha miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

‎Amesema kuwa Maabara hiyo inayotumia mfumo wa Makontena ambayo ni ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki iliyoanzishwa na taasisi ya FLI.

‎Dkt. Haroun ameeleza kuwa maabara hiyo inategemewa kutoa huduma za kiuchunguzi kwa viwango vya Ujerumani na Kimataifa kwa ujumla ambayo itatumia mifumo ya Tehama  itakayowasiliana moja kwa moja na Maabara kuu ya FLI ya Ujerumani.

‎Ameeleza kuwa Serikali inaendelea kufanikisha dhamira yake ya kuwaletea wananchi maendeleo kupitia sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya Kilimo na Mifugo ili kuwawezesha wananchi kujiua kiuchumi na kujiletea maendeleo.

‎Vile vile amefahamisha kuwa Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar inatambua na kuthamini juhudi na mchango uliotolewa kupitia Taasisi ya Utafiti wa Mifugo ya Ujerumani Friedrich-Loeffler-Institut (FLI).

‎Nae Naibu Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Dkt. Salum Soud Hamid, amesema mifugo ni moja ya sekta muhimu ya kiuchumi kwa wananchi wa vijijini ambao ni chanzo kikuu cha kujipatia kipato na chakula.

‎Ameeleza kuwa Sekta hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita imekuwa ikichangia asilimia 12 ya jumla ya sekta ya kilimo asilimia (24.3) ya pato la Taifa.

‎Amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuleta na kuendeleza juhudi za maendeleo kupitia sekta mifugo na kuleta mageuzi kwa kuzingatia matumizi ya teknolojia za kuongeza uzalishaji, tija pamoja na kuimarisha miundombinu ya uzalishaji.

‎Amefafanua kuwa Maabara hiyi italeta faida na manufaa kwa wafugaji, wakulima na wadau wa sekta ya misitu hususan kwa upande wa wanyama pori, kutokana na kuathirika kwa afya za wanyama hao kwa maradhi na kuhitaji kuchanjwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here