M
Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuwa Amani ya Nchi ndiyo hoja ya kwanza ya msingi ya Chama Cha Mapinduzi.
Amesema wananchi wana wajibu wa kuhakikisha amani inadumu kwani ndiyo msingi wa maendeleo yote, na ameahidi kuisimamia amani iliyopo kwa dhati.

Dkt. Mwinyi ameahidi yafuatayo katika mkutano huo:
- Serikali itaendelea kuimarisha na kudumisha Amani, Umoja na Maridhiano Zanzibar.
- Serikali itaendelea kuboresha Sekta ya Elimu na kujenga Skuli za kisasa zaidi.
- Huduma ya Maji itapatiwa suluhisho la kudumu kwa wananchi wote.
- Kukamilisha Ujenzi wa Bandari ya Wete na Bandari ya Shumba.
- Kujenga Barabara zote kuu na zile za ndani katika muda mfupi ujao.
- Kuongeza Pensheni ya Jamii kwa Wazee na Wastaafu.
- Kuwawezesha Wanawake wanaolima Mwani kwa Mikopo isiyo na riba na mazingira bora ya kazi.
- Kutoa hati za mashamba ya karafuu kwa wananchi na kuliimarisha zao la Karafuu kwa uchumi wa Taifa.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipokutana na mamia ya wanachama wa CCM na wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba katika mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Michezo wa Msuka, uliowakutanisha wavuvi, wajasiriamali, mama lishe, waendesha bodaboda, akinamama na wajane.
Mkutano huo pia umeshuhudia wanachama 364 wa ACT-Wazalendo kujiunga na CCM na kula kiapo cha utii, wakikabidhi kadi zao kwa Dkt. Mwinyi kama ishara ya kuunga mkono uongozi unaoleta maendeleo na maridhiano.






















