Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi ameuzindua Mji wa Dkt, Hussein Mwinyi uliopo Mombasa Zanzibar na kuutaka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii( ZSSF) kujikita katika Miradi mikubwa zaidi yenye tija kwa Nchi.
Rais Dķt, Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 23 Disemba 2025 alipouzindua Mji huo uliopo Mombasa, Mkoa wa Mjini Magharibi ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais Dķt, Mwinyi amefahamisha kuwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ndio inayoleta Maendeleo katika Nchi nyingi Duniani na kuipongeza ZSSF kwa Kuanza Vizuri kwa Ujenzi wa Mji huo wa kisasa.
Ameishauri ZSSF kujikita kuwekeza katika Miradi mikuwa ikiwemo Miradi ya Nishati ya Umeme baada ya Kufanya vizuri katika Ujenzi wa Masoko ,Vituo vya Mabasi na Nyumba za Makaazi.

Rais Dķt, Mwinyi amesema wakati Umefika kwa Zanzibar kuwa na Miji Mipya ya kisasa yenye haiba na iliyo Bora na kuona Wananchi wanaishi katika Makaazi Bora na mazingira Salama.
Ameeleza kuwa Bado Wananchi wengi hapa Nchini wanaishi katika Makaazi duni ,Mitaa isiyopimwa na kukosa Mipango miji na hali isiyoridhisha na kuwahimiza Wananchi kubadilika.
Aidha ametoa wito kwa Wananchi kuwa tayari kwa Mabadiliko pale Serikali inapoamua kutekeleza Miradi mikubwa ya Ujenzi wa Nyumba za Makaazi na Mipango ya Maendeleo kwa kuunga mkono juhudi na kuwahakikishia kuwa hakuna Mwananchi atakayedhulumiwa haki yake baada ya Kutoa eneo lake kupisha Utekelezaji wa Mradi.
Rais Dķt Mwinyi, ameupongeza Umoja wa Watu Wenye Ulemavu Zanzibar (UWZ)kwa kukubali kupisha Mradi huo kwa kuliachia eneo hilo lililokuwa likimilikiwa na Umoja huo. kwa ZSSF kutekeleza Mradi huo.
Uzinduzi huo wa Nyumba za gharama nafuu umeenda sambamba na uzinduzi wa Msikiti Mpya uliojengwa katika eneo hilo wa Masjid Balad Salaam.

Rais Dķt, Mwinyi ametoa wito kwa ZSSF na Waakazi wa Mji huo.wa Dkt, Hussein Mwinyi kuzitunza Nyumba hizo kwa kila mmoja kutoa Mchango wake ili ubaki na haiba yake kwa muda mrefu.
Rais Dķt, Mwinyi ameridhia Ombi la ZSSF la kupatiwa eneo kwa ajili ya Ujenzi wa Afisi katika eneo la.Mji wa Serikali wa Kisakasaka na kuiagiza Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi kuipatia Taasisi hiyo eneo la Ardhi kwa ajili ya Ujenzi huo na kuitaka ZSSF kujenga jengo litakalokuwa Bora na la mfano.
Waziri wa Fedha Dkt, Juna Malik Akili Amempongeza Rais Dkt, Mwinyi kwa kutekeleza kwa Vitendo Mambo yote anayoyaahidi kwa Wananchi anaowaongoza na kuthibitisha dhana ya Uongozi unaoacha Alama.
Akitoa taarifa ya Kitaalamu ya Mradi huo Katbu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt, Rahma Salim Mahfoudh amesema Mradi umegharimu Shilingi Bilioni 34 ,Ukiwa na Majengo 14 yenye ghorofa 5 kila moja yakiwa na Nyumba 276 za kisasa .umejengwa na Kampuni ya CRJE ya China .





















