Home Siasa RAIS MWINYI ATEUA WENYEVITI WA BODI MBALIMBALI ZA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

RAIS MWINYI ATEUA WENYEVITI WA BODI MBALIMBALI ZA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

21
0

Na Said Khamis, Desemba 22, 2025.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi mbalimbali katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, uteuzi unaolenga kuimarisha ufanisi wa taasisi za umma na kusimamia vyema utekelezaji wa majukumu yake ya kisheria na maendeleo.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Ofisi ya Baraza la Mapinduzi, Rais Dkt. Mwinyi amemteua Ndugu Makame Hasnuu Makame kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usafiri Zanzibar (ZMA). Ndugu Makame kwa sasa ni Mkurugenzi Mwendehaji wa Shirika la Meli na Uwakala Zanzibar (SHIPCO).

Aidha, Ndugu Sultan Said Suleiman ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), ambapo ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Zanzibar (ZHC).

Katika uteuzi mwingine, Ndugu Juma Burhan Mohamed ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA). Ndugu Juma ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar (ZEEA).

Vilevile, Dkt. Maudline Cyrus Castico ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), ambapo ni Waziri wa Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Pia, Dkt. Idrissa Muslim Hija ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Karakana Zanzibar. Dkt. Idrissa ni Katibu Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa uteuzi huo unaanza rasmi tarehe 22 Disemba, 2025, na unatarajiwa kuimarisha usimamizi, uwajibikaji na ufanisi wa taasisi hizo katika kutoa huduma kwa wananchi na kuchangia maendeleo ya Zanzibar kwa ujumla.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here