Home Siasa HILI HAPA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI SERIKALI YA YA NAPINDUZI YA ZANZIBAR.

HILI HAPA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI SERIKALI YA YA NAPINDUZI YA ZANZIBAR.

30
0

Na Mwandishi wetu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametangaza uteuzi wa Mawaziri na Manaibu Mawaziri wateule katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, hatua inayolenga kuongeza kasi ya maendeleo katika kipindi cha pili cha Awamu ya Nane ya uongozi wake.

Akizungumza leo tarehe 13 Novemba 2025, katika Ikulu ya Zanzibar, Dkt. Mwinyi amesema kuwa katika awamu hii Serikali itakuwa na wizara 20 badala ya 18, ili kuongeza ufanisi wa utendaji na kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Rais Dkt. Mwinyi amesisitiza kwamba uteuzi huo umezingatia vigezo vya weledi, uadilifu na uzingatiaji wa maslahi mapana ya Taifa, sambamba na kuhakikisha uwiano wa kijinsia na uwakilishi wa Visiwa vya Unguja na Pemba unazingatiwa.

Ameeleza pia kuwa wizara nne ikiwemo Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Wizara ya Afya, Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale, na Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda zitaachwa wazi kwa muda, hadi pale Serikali itakapokamilisha makubaliano na Chama cha ACT Wazalendo kuhusu uundwaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Katika uteuzi wa baraza hilo, Rais Dkt. Mwinyi amewataja mawaziri wateule kama huwa ni hawa wafuatao:

  1. Dkt. Haroun Ali Suleiman – Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora
  2. Dkt. Saada Mkuya Salum – Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Ikulu
  3. Dkt. Juma Malik Akil – Waziri wa Fedha na Mipango
  4. Idrissa Kitwana Mustafa – Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ
  5. Shariff Ali Shariff – Waziri wa Kazi na Uwekezaji
  6. Hamza Hassan Juma – Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi
  7. Rahma Kassim Ali – Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi
  8. Lela Mohamed Mussa – Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali
  9. Shaaban Ali Othman – Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji
  10. Suleiman Masoud Makame – Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo
  11. Nadir Abdullatif Alwardy – Waziri wa Maji, Nishati na Madini
  12. Masoud Ali Mohamed – Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi
  13. Dkt. Khalid Salum Mohamed – Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi
  14. Anna Athanas Paul – Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
  15. Mudrik Ramadhan Soraga – Waziri wa Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu
  16. Riziki Pembe Juma – Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amewateua Manaibu Mawaziri wafuatao:

  1. Badria Atai Masoud – Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi
  2. Dkt. Hamad Omar Bakari – Naibu Waziri wa Fedha na Mipango
  3. Ali Abdulgullam Hussein – Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo
  4. Zawadi Amour Nassor – Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
  5. Salha Mohamed Mwinjuma – Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi
  6. Seif Kombo Pandu – Naibu Waziri wa Maji, Nishati na Madini
  7. Dkt. Salum Soud Hamid – Naibu Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo
  8. Mboja Ramadhan Mshenga – Naibu Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi
  9. Mohamed Sijamini Mohamed – Naibu Waziri wa Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu
  10. Hassan Khamis Hafidh – Naibu Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji
  11. Khadija Salum Ali – Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali

Aidha Rais Dkt. Mwinyi amehitimisha hotuba yake, kwa kuwataka viongozi hao wapya kufanya kazi kwa bidii, kuonesha uzalendo, na kuweka mbele maslahi ya wananchi wote wa Zanzibar, akisisitiza kuwa Serikali yake imejipanga kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kuongeza ajira, na kuboresha maisha ya wananchi vijijini na mijini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here