Na Said khamis, Nov.12,2025.
Wavuvi wanaovua katika bahari ya Michamvi wametakiwa kufuata sheria na kanuni zilizowekwa na Idara ya Uvuvi na Maendeleo ya Mazao ya Baharini ili kuepusha migogoro na sintofahamu baina yao na wakazi wa shehia hiyo.
Ushauri huo umetolewa na Mjumbe wa Kamati ya Uvuvi ya Shehia ya Michamvi, Subira Idrisa Mwazini, wakati akizungumza na Mwanahabari wa TOZ huko Michamvi, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja.

Bi. Subira amesema kuwa serikali inaruhusu wavuvi kufanya shughuli zao sehemu yoyote ya bahari mradi tu wanazingatia sheria na taratibu zilizowekwa, isipokuwa pale wanapojihusisha na uvuvi haramu. Hata hivyo, aliwataka wavuvi kutoka shehia jirani kuheshimu utaratibu na mipaka iliyowekwa na wakazi wa maeneo wanapofanyia shughuli hizo, ili kuondoa migogoro na kuweka mahusiano mazuri kati ya wavuvi na jamii husika.
“Huwezi kumchukulia mtu hatua kwa sababu tu amevua katika bahari ya Michamvi au sehemu nyingine yoyote, hasa kama uvuvi huo ni halali. Tukifanya hivyo, hata sisi kama kamati ya uvuvi tunakuwa tumekiuka sheria,” alisema Subira.
Ameongeza kuwa malalamiko makubwa kutoka kwa wananchi wa Michamvi ni juu ya wavuvi kutoka shehia jirani wanaovua hadi kwenye maeneo yaliyotengwa kwa matumizi ya wakazi wa eneo hilo pekee, jambo linalozua kero na migogoro.

Aidha, ameomba kamati za uvuvi za shehia jirani kutoa elimu kwa wavuvi wao juu ya maeneo sahihi ya kuvulia, kulingana na mipango na makubaliano yaliyowekwa na wanakijiji, ili kuhakikisha kila upande unanufaika na rasilimali za bahari kwa usawa.
Kwa upande wao, baadhi ya wananchi wa Shehia ya Michamvi wamelalamikia tabia ya baadhi ya wavuvi kutoka shehia jirani kuvua hadi kwenye maeneo ya uso wa bahari ambayo wao huihifadhi kwa ajili ya wavuvi wadogo wadogo wa eneo hilo.
“Huku pwani ndiko kunako maisha yetu; hapa ndipo tunapopata riziki za familia zetu. Wavuvi wanapotoka maeneo mengine na kuja kuvua hapa, sisi tunakosa kipato cha kujikimu,” walisema wananchi hao.
Wamesema pia kuwa wavuvi hao wakati mwingine huwahatarishia usalama wa maisha yao, jambo linalowatia hofu kila wanapowaona wakifanya shughuli za uvuvi katika maeneo yao ya karibu.






















Kha uyo pweza,.
товары для дома магазин фиксированных цен https://oneprice.shop/
https://google.co.zm/url?q=http://oneprice.shop