Home Uchumi Biashara MFUMUKO WA BEI WAPUNGUA ZANZIBAR KUFIKIA ASILIMIA 0.06 MWEZI OKTOBA 2025

MFUMUKO WA BEI WAPUNGUA ZANZIBAR KUFIKIA ASILIMIA 0.06 MWEZI OKTOBA 2025

40
1

Na Rukaiya Juma, Nov. 11, 2025

Mfumko wa bei wa bidhaa za vyakula kwa mwezi Octoba mwaka huu umeongezeka na kufikia asilimia 6.41 ikilinganishwa na asilimia 4.13 iliorikodiwa kwa mwezi Septemba mwaka huu.

Akiwasilisha takwimu za mfumko wa bei za bidhaa mtakwimu katika kitengo cha takwimu za bei kutoka ofisi ya mtakwimu mkuu wa Serekali ndugu Hassan Jamal Hassan amesema kuwa kwa mwezi wa Oktoba 2025 mfumuko wa bei umeongezeka hadi kufikia asilimia 0.06 ikilinganishwa na asilimia 0.21 iliyorikodiwa katika mwezi ulioishia Septemba  2025 ambapo sababu zilizopelekea kushuka kwa mfumuko wa bei wa mwezi ni pamoja bidhaa za samaki (7.41%)Sukari nyeupe (0.79%)mafuta ya disel(1.64%)mafuta ya petrol(4.55%).

Sambamba na hayo ameeleza kuwa mfumko wa bei wa bidhaa za chakula wa mwaka ulioishia mwezi Oktoba 2025 umeongezeka na kufikia asilimia 6.41 ikilinganishwa na asilimia na asilimia 4.13 iliyorikodiwa katika mwezi wa septemba 2025.Ambapo faharisi za bei za bidhaa za chakula kwa mwezi wa Oktoba 2025 zimeongezeka na kufikia 129.96 kutoka 122.13 iliyorikodiwa katika mwezi wa oktoba 2024.

Mfumko wa bei wa bidhaa zisizokuwa za chakula kwa mwaka umepungua na kufikia asilimia 1.04 kwa mwezi wa oktoba 2025 ikilinganishwa na asilimia 2.93 iliyorikodiwa katika mwezi wa septemba 2025.

Wakiwasilisha michango yao wadau katika kikao hicho wamesema kuwa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ina mpango wa kujenga maghala ya kuhifadhia chakula ili kuhakikisha inadhibiti mfumko wa bei usiweze kuathiri katika nchi pamoja na kuhamasisha uzalishaji sambamba na kupunguza kodi kwa wafanyabiashara.

Naye Meneja wa Uchumi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Ofisi ya Zanzibar, Moto Ng’winganale Logobi, amesema kuwa kupungua kwa thamani ya dola ya Marekani dhidi ya shilingi ya Kitanzania kumechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama za manunuzi ya bidhaa mbalimbali zinazoagizwa kutoka nje ya nchi.

Aidha Amesema mabadiliko hayo yameleta nafuu kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla, kwani gharama za uagizaji wa bidhaa muhimu kama vile mafuta, chakula, na vifaa vya ujenzi zimeanza kushuka, jambo linalosaidia kupunguza shinikizo la mfumko wa bei katika soko la ndani.

Kwa upande wake Kamishna mipango wa Tume ya Mipango Zanzibar Mohamed Salim amesema mfumko wa bei unaweza kupungua iwapo kutakuwepo na bidhaa za kutosha ikiwa kuna uhifadhi mzuri wa bdhiaa kwa kipindi Fulani.

Hata hivyo amesema uwepo wa bidhaa za ndani inasaidia kupunguza mfumko wa bei za bidhaa ambazo zinaingizwa nchini kwani husaidia kukidhi mahitaji ya wananchi.

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here