Na Siti Ali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewahimiza wananchi kuendeleza utaratibu wa kuiombea nchi amani ili mipango mbalimbali ya maendeleo iweze kutekelezwa kwa mafanikio.
Alhaj Dkt. Mwinyi ametoa rai hiyo leo tarehe 07 Novemba 2025 alipojumuika na waumini wa dini ya Kiislamu kwa Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Ijumaa, Malindi.
Amesema kuwa baada ya kufanikiwa kukamilisha Uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu, ni wajibu wa kumshukuru Mwenyezi Mungu na kuendelea kumuomba ili amani hiyo idumu.

Aidha, amefahamisha kuwa kazi nzuri iliyofanyika kabla na wakati wa uchaguzi katika kuiombea nchi amani, inapaswa kuendelezwa kwa juhudi kubwa zaidi.
Alhaj Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa ni neema kubwa kwa nchi kubaki na umoja, amani, utulivu na mshikamano baada ya uchaguzi, na amewasisitiza viongozi wa dini pamoja na waumini kuendelea kuiombea nchi ibaki salama wakati wote






















