Home Jinsia TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR YATEUA WAJUMBE WA VITI MAALUM VYA WANAWAKE...

TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR YATEUA WAJUMBE WA VITI MAALUM VYA WANAWAKE 2025.

37
0

Na siti Ali.

Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imetangaza uteuzi wa wajumbe wa Viti Maalum vya Wanawake katika Baraza la Wawakilishi kufuatia kukamilika kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliofanyika tarehe 29 Oktoba 2025. Uteuzi huo ulifanyika katika kikao cha Tume kilichofanyika tarehe 4 Novemba 2025, kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 67(1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 pamoja na kifungu cha 55(3) cha Sheria ya Uchaguzi Nam. 4 ya mwaka 2018.

Katika uteuzi huo, jumla ya wajumbe 20 wameteuliwa kuwakilisha wanawake katika Baraza la Wawakilishi, ambapo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa wajumbe 16, na chama cha ACT Wazalendo kimetoa wajumbe 4. Mgawanyo huo umetokana na asilimia ya viti vya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi vilivyopatikana na kila chama katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Wajumbe walioteuliwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni Zainab Khamis Shomari, Rahma Kassim Ali, Tabia Maulid Mwita, Fatma Ramadhan Mandoba, Riziki Pembe Juma, Maryam Said Khamis, Chumu Khamis Kombo, Lela Muhamed Mussa, Khadija Salum Ali, Zainab Abdalla Salum, Anna Athanas Paul, Aza January Joseph, Salha Moh’d Mwinjuma, Hudhaima Mbarak Tahir, Mwanaidi Kassim Mussa na Salma Mussa Bilali.

Aidha Kutoka chama cha ACT Wazalendo, walioteuliwa ni Moza Mohamed Khamis, Jabu Makame Juma, Farida Amour Mohamed na Nassra Nassor Omar.

Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar imesisitiza kuwa uteuzi huu umezingatia uwiano wa uwakilishi wa kijinsia unaolenga kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi na maamuzi ndani ya Baraza la Wawakilishi, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa matakwa ya Katiba na Sheria za Uchaguzi za Zanzibar.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here