Na Fatma Hamad, Pemba.
Kukosekana kwa ruzuku ya pesa kwa ajili ya kufanyia kampeni za uchaguzi mkuu 2025, imekua ni kikwazo kikubwa kinachorudisha nyuma ndoto za kufikia uongozi wagonbea kisiwani pemba.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Maryam Saleh Juma mgombea Ubunge jimbo la Ole chama cha Ukombozi wa Umma alisema kukosekana kwa ruzuku za kufanyia kampeni imekua ni changamoto inayopelekea kukosa kufanya mikutano ya kampeni.
Amesema kukosa kufanya mikutano ya hadhara katika majimbo yao ni kikwazo kwao kwani, wanashindwa kutangaza sera zao wananchi wakawatambua na kufanya maamuzi ya kuwachagua.

Amesema anachokifanya yeye ni kupita nyumba hadi nyumba na kuomba kura, kwa vile hakua na pesa ya kufanyia mikutano.
‘’Sijabahatika kufanya mkutano hata mmoja wa hadhara, wala kutoa kipeperushi, napita tu majumbani nikiomba kura, jee unadhani wananchi wote watanifahamu na kunipa kura zao,’’amesema.
Kwa upande wake Asha Mohamed Ali mgombea Ubungejimbo la Wawi kupitia Chama cha UDP, alisema walifanya mkutano mmoja tu wa hadhara siku ambayo mgombea wao wa Urais wa Jamuhuri ya Mungano alipokuja kisiwani Pemba.
Amesema kampeni zake maranyingi ni kupita nyumba hadi nyumba na kuomba kura.
‘’Tulibahatika kufanya mkutano mmoja tu wahadhara siku alipokuja mgombea wetu wa Urais wa Muungano, ila kwa mimi sijafanya hata mmoja.
Aidha amesema amebahatika kutoa vipeperushi kidogo na kuvisambaza katika jimbo lake, wananchi wapate kuzifahamu sera zake.
Nae Rahma Omar Hamad mgombea Ubunge jimbo la Wete kwa tiketi ya chama cha ADC amesema hata chama chao hawakupata ruzuku, isipokua Mgombea wao wa Urais ndie aliebeba jukumu la kuwasaidia na kufanya mikutano ya hadhara.

Amesema ni vyema kwa viongozi wa vyama vya siasa kuhakikisha ruzuku wanazozipata kwa ajili ya kufanyia mikutano ya kampeni kuwasaidia na wagombea wao wa majimbo wafanye mikutano kwenye majimbo yao.
Mgombea Uwakilishi kwa tikaeti ya Chama cha Mapinduzi CCM jimbo la Tumbe Salma Khamis Tumu amekishukuru chama chake kwani, kimempatia fedha ambazo zimemsaidia kufanya mikutano yake ya kampeni, na masuala mengine yanayohusiana na uchaguzi.
‘’Ijapokua tulichelewa kupata fedha lakini tulipoingiziwa tu tuliendelea kufanya kampeni tukanadi sera zetu vizuri nashukuru zimeniwezesha, hivyo nawaomba wananchi wanichague, nilete maendeleo jimboni kwetu,, alisema,’’Salma.
Mwenyekiti wa Chama cha ADA TADEA Wilaya ya Wete Mohamed Khamis Hamad amesema, ukosefu wa ruzuku unawakwaza wagombea wanawake, jambo ambalo linaweza kuwafelisha.
Nae Naibu Katibu Mkuu Zanzibar wa Chama cha Ukombozi wa Umma CHAUMA Mohamed Masoud Rashid amesema katika chama chao hakuna mgombea hata mmoja aliepata ruzuku, ingawa waliomba serikali wawasaidie angalau wanawake tu, lakini ilishindikana.
Mkurugenzi wa Chama cha Wandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Zanziba Mzuri Issa Ali ameeleza kuwa, wanawake ni kundi maalumu ambalo kwa miaka mingi limeachwanyuma, ambapo alivishauri vyama vyote view na sera ya kijinsia ambayo wataitekeleza ipasavyo na sio kuepo tu.
‘’Moja kati ya jambo muhimu ni kuwatambua wanawake ambao wanahitaji uongozi na kuwapa hizo nafasi na jengine ni kuwapa mashirikiano ya hali na mali, ili kuweza kutekeleza mambo ya uongozi vizuri,’’anafafanua.

Dr Mzuri amesema ikiwa wagombea hao hawahupata ruzuku hiyo ni bahati mbaya sana na ni mapungufu makubwa kwa vyama vya siasa, kwani walivishauri mwanzo kwa vile vyama vinavyopata ruzuku viweke fungu maalumu, na ambavyo havipati vijue kwamba hilo jambo lipo vianze kutafuta fedha mapema kuhakikisha wanawake hawapati shida kutokana na fedha.
Nae Msaidizi wa Vyama vya siasa Tanzania kwa upande wa Zanzibar Sisty Nyhoza, amesema sio vyama vyote vya siasa vinapewa ruzuku kipindi cha kampeni na uchaguzi.
Alisema kuwa, ili chama kipewe ruzuku ni lazima kiwe na Mbunge au Muwakilishi katika uchaguzi uliopita na wala hakuna ruzuku kwa wagombea wanawake wala wanaume.
‘’Kiukweli hatutoi ruzuku kwa mgombea mwanamke wala mwanamme, isipokua chama kiwe na Mbunge na Mwakilishi katika uchaguzi uliopita,’’amefafanua.
Chama chenye usajili kamili kinahaki ya kupata ruzuku endapo kina mbunge au diwani wa kuchaguliwa na kimetimiza masharti ya kupata ruzuku, yaliyomo katika Sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 kama ilivyomarekebisho ya mwaka 2024.
Kwa mfano kuwa na Akaunti ya benki (kifungu cha 15(2), hesabu zake kukaguliwa na CAG (kifungu cha 14(1)(b)(i) na kutumia fedha za ruzuku kwa mujibu wa sharia ya vyama vya siasa inavyoelekeza(kifungu cha 18).





















