Home Jamii ADC YAAHIDI MABADILIKO KWA WANAJIMBO LA WAWI.

ADC YAAHIDI MABADILIKO KWA WANAJIMBO LA WAWI.

24
0

Na Fatma Hamad, Pemba.

MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) Hamad Rashid Moh’d amesema  endapo atachaguliwa na kuingia madarakani atahakikisha  rasilimali ardhi zinatumiwa na wazawa wenyewe, ili wafanyie shughuli zitakazowaletea maendeleo.

 Mgombea huyo ameyasema hayo wakati akifunga kampeni katika viwanja vya Wawi ditia wilaya ya Chake chake mkoa wa Kusini Pemba.

Amesema endapo kutakua na ardhi yoyote itakayo tumika kwa ajili ya kupisha ujenzi wa miundombinu kama bara bara, wananchi watatengewa maeneo mengine, wafanye shughuli zao za uzalishaji bila shida yoyote.

   ‘’Naahidi nitahakikisha mashamba yenu na ardhi zenu mutazitumia nyinyi wazawa wenyewe, kama ni kukodisha  mtu atakodisha mwenyewe na kwa bei anayotaka mwenyewe,’’amesema.

Aidha amesisitiza kuwa ataweka ruzuku maalumu kwa wanawake wajane ambao wamefiwa ama wameachwa na waume zao.

Sambamba na hilo ameahidi kuwasaidia mahari wanaume watakaojitolea kuwaoa wanawake hao wajane, ili amsitiri mama huyo pamoja na watoto wake.

Kwa upande wake mgombea ubunge wa jimbo la Wawi kupitia chama cha ADC Mahmoud Rashid Mohamed amesema akichaguliwa ataboresha miundombinu ya maji, ili wananchi waondokane na kadhya na usumbufu wa upatikanaji wa maji safi na salama kwa urahisi na endelevu.

Pia amesema akichaguliwa atanzisha vitalu vya miche mbali mbali ya kilimo kwa wajasiriamali na wakulima, ili kusaidia kupatikana kwa ajira kwa vijana wa Wawi.

Nae mgombea udiwani Raya Khatib Juma amewataka vijana wasikubali kushawishiwa na baadhi ya wanasiasa kwa kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani katika kipindi cha uchaguzi.

‘’Niwaombe nduguzangu mkishamaliza kupiga kura  rudini majumbani mwenu mtulie, msije mkafanya vurugu, jambo litalopelekea migongsno nchini,’’ameshauri.

Mkutano huo wa kufunga kampeni umekuja ili kupisha uchaguzi mkuu tarehe 29 Oktoba 2025, ambapo wananchi watatekeleza haki yao ya kikatiba kuchagua viongozi kwa ngazi ya uwakilishi Udiwani, Ubunge na Urais.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here