Home Uchumi Fedha MGOMBEA KIWANI AAHIDI KUINUA KUINUA MADRASA NA KUWEKA MASHINDANO YA QUR-

MGOMBEA KIWANI AAHIDI KUINUA KUINUA MADRASA NA KUWEKA MASHINDANO YA QUR-

27
0

Na Siti Ali.

Mgombea wa Uwakilishi Jimbo la Kiwani, Mhe Hemed Suleiman Abdulla, amesema akipewa ridhaa na wananchi kuwa Mwakilishi wa Jimbo hilo, ataipa kipaumbele sekta ya elimu, hususan elimu ya madrasa, kwa kuhakikisha anazisimamia kwa karibu madrasa zote zilizomo ndani ya jimbo hilo.

Akizungumza na walimu wa madrasa za Jimbo la Kiwani wakati akiomba kura, Hemed amesisitiza kuwa atahakikisha suala la uhifadhi wa Qur-an kipaumbele kwa kushirikiana na viongozi wa dini na jamii.

Ameasema, katika juhudi hizo, ataweka mashindano ya kuhifadhi Qur-an mara mbili kwa mwaka, au kulingana na makubaliano na walimu wa madrasa, na kwamba mwanafunzi atakayefanya vizuri zaidi atazawadiwa zawadi yenye heshima na thamani inayoendana na kitabu kitukufu cha Qur-an.

“Ni lazima tuweke mazingira bora ya kujisomea, kuboresha maslahi ya walimu na kuwapatia vifaa vya kisasa vya kufundishia ili wanafunzi waweze kuhifadhi Qur-an kwa ufanisi bila changamoto,” amesema  Hemed.

Aidha, amebainisha kuwa atahakikisha wanafunzi wa madrasa wa Jimbo la Kiwani wanashiriki katika mashindano ya tahfidh Qur-an ndani na nje ya Zanzibar bila ya vikwazo vyovyote, huku akiahidi kuwa walimu wa madrasa watapatiwa mikopo isiyo na riba ili kuwawezesha kujiongezea kipato na kuboresha maisha yao.

Sambamba na hilo,  Hemed amewataka walimu wa madrasa kutumia nafasi yao kuwahamasisha vijana kudumisha amani na utulivu hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.

“Amani ni jukumu la kila mmoja wetu, hivyo tuhakikishe tunaitunza na kushiriki kwa wingi siku ya uchaguzi, kuwachagua viongozi watakaoliletea maendeleo Jimbo la Kiwani na Zanzibar kwa ujumla,” amesisitiza.

Kwa upande wake, akizungumza kwa niaba ya walimu wa madrasa, Ustadh Mtumwa Mcha Haji anasema walimu wa madrasa wanakabiliwa na changamoto nyingi zinazowarejesha nyuma katika juhudi za kuhifadhisha Qur-an.

Amesema, miongoni mwa changamoto hizo pamoja na upungufu wa vifaa vya kufundishia na uhaba wa mafunzo maalumu ya kufundisha tahfidh, ili kuwaandaa walimu wenye ujuzi wa kina wa Qur-an Tukufu.

“Tunaamini atakapochaguliwa, Ndugu Hemed ataweka nguvu kubwa katika kuinua elimu ya madrasa na kuimarisha malezi ya kiroho kwa watoto wetu,” anasema Ustadh Mtumwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here